UTANGULIZI
Maana ya Neno kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali........................
Kiini
Ugumu wa kufasili dhana ya neno...........….
Hitimisho.................................................
Marejeo.
Neno,ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandkiwa na kuleta maana (TUKI 2004).
Neno linaweza kufafanuliwa katika misingi ya kiumbo-sauti (yaani sauti zinazounda umbo zima)Kiotografia (yaani kuchunguza herufi zinazotumika katika kuliandika umbo lake) na kisarufi (yaani kuchunguza kile kilichowakilishwa na umbo husika katika lugha) (Kihore na wenzake 2012).
Neno ni udhihiriko halisi wa leksimu ama kwa mazungumzo au maandishi kwa maana ya umbo fulani la nen, pia Neno ni kiwakilishi cha leksimu ambayo inahusiana na masuala ya kimofosintaksia kama nomin,Kivumishi na Idadi ya njeo ( Katamba 1993).
Neno linaweza kuwa kipashio cha kiisimu kinachoundwa na maana moja au zaidi, Dhana ya neno ni tata mno hasa katika kubainisha vipashio vingine katika lugha.(Habwe na karanja 2004).
Neno linaweza kufafanuliwa katika misingi ya kiumbo-sauti (yaani sauti zinazounda umbo zima)Kiotografia (yaani kuchunguza herufi zinazotumika katika kuliandika umbo lake) na kisarufi (yaani kuchunguza kile kilichowakilishwa na umbo husika katika lugha) (Kihore na wenzake 2012).
Neno ni udhihiriko halisi wa leksimu ama kwa mazungumzo au maandishi kwa maana ya umbo fulani la nen, pia Neno ni kiwakilishi cha leksimu ambayo inahusiana na masuala ya kimofosintaksia kama nomin,Kivumishi na Idadi ya njeo ( Katamba 1993).
Neno linaweza kuwa kipashio cha kiisimu kinachoundwa na maana moja au zaidi, Dhana ya neno ni tata mno hasa katika kubainisha vipashio vingine katika lugha.(Habwe na karanja 2004).
Kwa mujibu wa kundi (Reuben sabsteka, Ilomo Guntram, Mwigulu mapembe, Oliva,Nikwininga,winie,Sophia,District,Mary) Tunafasili dhana ya neno kama ,Ni muunganiko wa irabu na irabu au irabu na silabi ambapo ukitamkwa kwa pamoja huleta maana. Mfano wa irabu na irabu ni o+a= oa.pia mfano wa silabi na irabu ni k+a+k+a =kaka.
Dhana ya neno imefasiliwa na wataalamu mbalimbali; Ni kweli kwamba dhana ya neno ni tata katika kuifasili, Utata huo umetokana na vigezo mbalimbali vya kisarufi ambavyo wanaisimu huvitumia kama mwongozo katika kufasili dhana hii. Miongoni mwa vigezo hivyo ni kama vifuatavyo :-
Kigezo cha kifonolojia; Neno ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa (TUKI 1990),Silabi hizo huwa tofauti kutoka lugha moja hadi nyingine.Mfano katika lugha ya kiswahili neno "karibu" lina silabi tatu (3)$ ka $$ ri $$ bu $ kwa kigezo hiki pia huweza kufafanuliwa kama vipande vya matamshi yaani fonimu zinazopangwa katika mpangilio maalumu ili zilete maana . Mfano neno bata lina fonimu nne (4) ambazo ni /b/a/t/a/ Mpangilio huu ukigeuzwa maana ya meno pia hubadilika na watumiaji wa lugha hiyo hawataelewa maana ya neno hilo .Mfano neno *taba* japokuwa limeundwa na fonimu zilezile lakini halina maana kwa sababu mpangilio huo haupo katika lugha ya kiswahili.
Vilevile kwa mujibu wa mtandao (chomboz.blogspot.com) katika lugha ya kiingereza ,Sifa itumikayo kuonyesha kuwa hili ni neno ni "Mkazo msingi" ambao huwa ni mmoja tu katika neno. Mfano "Rayvan is going to school" tungo hii ina maneno matatu ambayo ni "Rayvan" "going" na "school" kwa kigezo hik "is" na "to" si maneno. Kigezo hiki kinazingatia viambajengo vya lugha kama fonimu silabi na mkazo.
Kigezo hiki kinamapungufu hasa katika kipengele cha mkazo , kila lugha ina sheria zake katika uwekaji mkazo . Kwa mfano katika lughaya kiswahili Mkazo msingi huwekwa katika Silabi ya mwisho.kasoro moja na hatima kwenda katika neno la mwisho kila maneno yanapoongezeka katika tungo.
Mfano 1:-
Anakula.
Anakula chakula.
Anakula chakula kitamu .
Silabi iliyopigiwa mstari ina mkazo msingi huhama kadri maneno yanavyozidi kuongezeka.
Mfano 2:-
Baba.
Baba analima.
Baba analima shambani.
Neno la kwanzo mkazo wa msingi upo kwenye "ba" ya pili, Neno la pili mkazo wa msingi umehamia kwenye "li", Na neno la tatu umehamia kwenye " mba". Swali ni je! Kama neno katika kigezo hiki cha kimofolojia tunaangalia mkazo msingi haya maneno ambayo mkazo wake umehama sio maneno tena?
Pia kuna lugha kama kihehe kidigo ci-ruuri, lugha hizi hazina mkazo bali zina toni ( massamba 2010). Hivyo kwa kigezo cha mkazo ni vigumu kubainisha maneno katika lugha hizo.
Kigezo cha kisemantiki; Neno linafasiliwa kuwa ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana (mdee 1997). Kwa maana hiyo Neno ni lazima liwe na maana inayoeleweka na jamii inayotumia lugha hiyo.
Mfano: Mama - mzazi wa kike.
Ndama - mtoto wa ng'ombe.
Fasili hii ina mashiko kwa sababu maneno mengi katika lugha yana maana ya kueleweka kwa mtumiaji wa lugha hiyo lakini kwa upande mwingine si kila neno linalotumika linaweza kuwa na maana ya wazi au ya kisemantiki. Kwa mfano viunganishi kama na, ya, kwa, wakati,ambavyo na japokuwa havina maana ya kisemantiki lakini vina uamilifu kisarufi.
Kigezo cha kisintaksia; Wataalamu wa kigezo hiki wanafasili neno kama kipengele kidogo kabisa cha sentensi ambacho kinaweza kuhamishwa kutoka nafai moja hadi nyingine bila kuathiri sarufi ya lugha katika tungo au sentensi hiyo. (Cruse 1986) alinukuliwa na Mdee (1997). Kwa ujumla wataalamu hawa wanatazama zaidi kategoria za maneno na mpangilio wake katika lugha.
Mfano: Ali alimuua Ahmad.
N T N
Ahmad alimuua ali.
N- Nomino,T- ni kitenzi na N ya mwisho ni nomino japo zimebadilika lakini sarufi ya lugha hiyo haijaathirika.
Kwa ujumla utaratibu huu husaidia sana katika kujifunza sarufi ya lugha hasa miundo ya tungo kama virai, vishazi na sentensi na pia katika kujua sehemu za tungo kama vile kiima na kiarifu
Lakini kwa upande mwingine kigezo hiki kina upungufu sio maneno yote yanaweza kuhamishwa bila kuharibu sarufi ya lugha.
Mfano:
Alia amesimama kando ya mto.
Amesimama kando ya mto Alia.
Kando ya mto Alia amesimama.
* Mto Alia amesimama kando ya.
* Mto ya kando amesimama Alia.
Sentensi mbili za mwisho (zilizo wekewa nyota) Kwa sabubu hizikidhi hoja ya usahihi wa kisarufi kwa mujibu wa Mdee (1997).Vilevile unapohamisha maneno maana ya neno huweza kubadilika .
Kwa mfano:
(ⅰ) Zubeda anapenda zawadi.
(ⅱ)Zawadi anapenda zubeda.
Japokuwa Nomino katika sentensi hizo zimebadilishana nafasi haijaathiri sarufi ya lugha lakini kimaana imebadilika kwa sababu katika sentensi ya kwanza Zubeda ndiye aliyetenda tendo, na katika sentensi ya pili Zawadi ndiye anatenda tendo.
Kigezo cha kileksika; Neno ni dhana dhahania ya kileksikoni ambayo neo hurejerewa kama leksimu. Leksimu ni msamiati ulioorodheshwa kwenye kamusi ( Katamba 1993:17) Neno hili leksimu huwa na maana kimsamiati (TUKI 1990) Kwa kawaida leksimu huwa na vibadala vyake kutegemeana na leksimu yenyewe .
Mfano: Go - vibadala vyake ni going,went na goes.
Cheza - cheze,chezea,chezeana,mchezea.
Refu - refu,ndefu,mrefu,kirefu.
Dhana hii inasaidia katika taaluma ya mofolojia,Leksikografia na taaluma zinginezo, lakini bado inamapungufu au bado haijajitosheleza swali ni je!, maumbo yanayotokana na leksimu moja kama ilivyo katika maneno "cheza - chezea,chezeana,mchezea" na "refu - refu,ndefu, mrefu,kirefu ni maneno tofauti au ni neno moja? Pia kuna maumbo yenye umbo moja lakini yana maana tofauti haya nayo yatakuwa neno moja au maneno zaidi ya moja, Mfano " Paa"-mnyama, Paa- enda angani au enda juu, Paa - sehemu ya juu ya nyumba. Pia katika lugha kuna maneno ambayo yakisimama peke yake hayaleti maana na si leksimu katika kamusi lakini maneno hayo yakikurubishwa na maneno ya kileksimu yanaleta maana. Mfano:- katika lugha ya kiswahili kuna viunganishi kama na, ya, kwa na vitenzi vishirikishi (husishi) kama ni, si, _kuwa, na ndi_(ndiye, ndiyo n.k) ambavyo si leksimu lakini hufanya kazi ya leksimu kisarufi au vinauamilifu katika lugha.
Kigezo cha kiotografia;Neno linafasiliwa kama mfululizo wa herufi zinazofungamana pamoja na kuzungukwa na nafasi tupu ( Mdee 1997). Utaratibu wa kuweka nafasi hufuata taratibu maalumu za kiotografia ambazo hutofautiana kutegemeana na lugha moja hadi nyingine. Mfano katika lugha ya kiswahili, "Mama alirudi jana usiku", Tungo hii ina maneno manne (4) Yaani "Mama" "alirudi" "jana" na "usiku". Kwa ujumla ubora wa mkabala huu ni kwamba husaidia sana katika uandishi wa matini za kitaaluma hasa kwa lugha zinazofuata utaratibu huu. Lakini pia ina mapungufu kama kama ifuatavyo:-
Dhana ya nafasi tupu ipo tu kwenye maandishi inamaana kuwa tunapozungumzia nafasi tupu hatuachi nafasi tupu baina ya maneno tunayotamka yote kwa mfululizo.
Vilevile utaratibu wa kuweka nafasi mwanzoni au mwishoni mwa neno haupo katika lugha zote. Kuna lugha kama kigiriki na kieksimo maneno yake katika tungo hayawekewi nafasi tupu.kwa mfano katika tungo ifuatayo ya lugha ya kieksimo.
Mfano: "Kaipiallrullinink" Yenye maana ya kuwa " wote walikuwa na njaa" Tungo iliyowekwa katika herufi za italiki( hati mlazo) ni ya kieskimo ambayo haina nafasi kati ya neno moja na lingine. Pia kigezo hiki kinaupungufu kwamba hakiangalii viambajengo vinavyo jenga neno, kwa mfano Fonimu,Silabi, Mkazo na Toni.
Kutokana na fasili hizo tunaona kuwa kuna ugumu katika kufasili dhana ya neno ,Ugumu huo unasababishwa na sababu zifuatazo:-
Ugumu wa kufasili dhana ya neno unasababishwa na utofauti wa lugha kimaumbo,Kimatamshi, kimuundo na kimaana, Hivyo ni vigumu kuhusisha fasili moja inayoweza kuhusisha mifumo yote ya lugha kwa usahihi kwa sababu lugha hutofautiana katika vipengele hivyo ( spencer 1991).
Ugumu wa kufasili neno unatokana na mitazamo tofauti ya wanaisimu kuhusu kipashio hicho (Neno) kiotografia kina maumbo na kimatamshi. Hivyo kwa kuwa kila mwanaisimu anamtazamo wake hii inapelekea kuto kukubaliana maana moja ya neno.(Mdee 1997).
Ugumu wa kufasili dhana ya neno unatokana na utofauti wa utamaduni na mazingira na maarifa ya wanaisimu . Hii ndio sababu kila mtu anafasili neno kutokana nalugha yake iliyo na maarifa aliyonayo. Wanafonolojia wanafasili neno kwa kuzingatia nduni za fonolojia kama silabi, fonimu, toni, na mkazo, Wanaleksikografia wanafasili neno kama leksimu (chomboz.blogspot.com).
Kwa ujumla tunaweza kuhitimisha kwa kusema ugumu wa kufasili dhana ya neno umetokana na tofauti za wanaisimu kilugha, kitaaluma, kimazingira, kimtazamo na kiutamaduni. Hivyo basi ili kuondoa au kuziba upungufu wa kigezo kimoja, ni lazima vigezo zaidi ya kimoja vitumike katika kuangalia maana za maneno katika lugha tofauti.
MAREJEO
- KihoreY.M na wenzake(2012),Sarufi ya maumbo ya kiswahili sanifu (SAMIKISA),sekondari na vyuo,Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili (TUKI),Dar es salaam,Tanzania.
- Rubanza Y.I(1996),Mofolojia ya kiswahili, Chuo kikuu huria cha Tanzania,Msasani, Dar es salaam, Tanzania.
- Habwe.J & Karanja.P(2004),Misingi ya sarufi ya kiswahili ,Phoenix publishers ltd,Nairobi Kenya.
- OUP(T)ltd,East african & TUKI (2004), Kamusi ya kiswahili sanifu ,Oxford university press(T),Nairobi Kenya.
- Mdee.D (1977),Nadharia za leksikografia, TUKI,Dar es salaam Tanzania.
- Spencer.A(1991),mophological theory:An introduction to word structucture in generative grammer, blackwell.UK.
- Chomboz.blogspot.com/ugumu wa kufasili neno>2016/03.
Naomba kujua maana ya neno kisintakisia
ReplyDeleteNice material
ReplyDeleteNini maana ya neno kutayuka
ReplyDeleteBinafsi nakubali kazi zako. Endelea kutoa elimu stahiki.
ReplyDelete